‘Nishati ya Nyuklia Siyo Ufumbuzi wa Mabadiliko ya Hali ya Hewa’

AddThis

Nuclear Abolition News | IPS
Neena Bhandari anamhoji DK SUE WAREHAM, mpinzani wa matumizi ya nyuklia duniani


MELBOURNE (IPS) - Wakati tishio la silaha za nyuklia likizidi kuhatarisha maisha ya watu duniani, Dk Sue Wareham, mjumbe wa bodi wa Autralia wa Kampeni ya Kimataifa ya Kukomesha Matumizi ya Silaha za Nyuklia (ICAN), anatoa wito wa kukomeshwa kwa haraka kwa silaha hizo na kukataa nishati ya nyuklia kuwa ufumbuzi wa mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Akiongea katika mkutano wa kukomesha nyuklia na umilikaji wa silaha katika Bunge la Kidini Duniani mwaka 2009, Wareham alisema nguvu ya dini inapaswa kutumika pamoja kuleta amani katika dunia kupitia kukomeshwa umilikaji wa silaha, silaha za nyuklia, kutokomeza umaskini na kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Akiwa mtaalam wa utabibu na rais wa zamani wa Chama cha Madaktari cha Kuzuia Vita (MAPW) cha Australia, Dk Wareham ana imani kuwa kazi yake na MAPW ni muhimu kwa dhamira yake ya kulinda maisha na kuboresha ustawi wa mwanadamu.

Katika mahojiano na IPS, anaelezea kwa undani juu ya dhamira yake ya wito wa jamii isiyokuwa na silaha za nyuklia.

IPS: Ni kwa nini kuna uharaka wa kukomesha matumizi ya nyuklia sasa?

SUE WAREHAM: Moja ya sababu suala hili linakuwa la haraka ni kutokana na kwamba tathmini ya miaka mitano ya Mkataba wa Kuzuia Kuenea kwa Silaha za Nyuklia (NPT) itafanyika Mei 2010. Ni wazi kuwa kama hakutakuwepo na hatua za kupunguza silaha na dalili za wazi kutoka kwa mataifa yenye nyuklia kuwa yana nia ya kuchukua hatua ya kuondokana na silaha zao, hatutaweza kuzuia kuenea kwa silaha hizo zaidi. Hivyo kusitisha kumiliki silaha za nyuklia na kuzuia kuenea kwa silaha hizo vinapaswa kwenda pamoja.

IPS: Lengo la ICAN ni la Mkataba wa Silaha za Nyuklia, mkataba ambao unazuia ubunifu, kufanya majaribio, kuzalisha, kutumia na kutishia kutumia silaha za nyuklia. Je inawezekana kufikia lengo na ufumbuzi?

SW: Hakika inawezekana kufikia lengo, na ni muhimu. Tunawataka watu duniani kote kuweka shinikizo kwa serikali zao kutangaza Mkataba wa Silaha za Nyuklia katika mkutano wa tahmini ya NPT mwaka ujao. Tunaona mkataba kama wenye njia yenye matarajio mema kwa dunia kuchukua hatua ya kutokomeza silaha za nyuklia.

Tuna sheria zinazofanana katika nchi zote na hii imesababisha moja ya matatizo makubwa kwa sasa, ambalo ni kwamaba kuna sheria zinazofanana kwa nchi ambazo tayari zina silaha za nyuklia na sheria nyingine kwa nchi zisizokuwa na silaha hizo.

IPS: Ni kwa nini ubinadamu umekwenda polepole mno na kukosa ufanisi katika kufikia changamoto inayotokana na silaha za nyuklia?

SW: Mataifa ambayo yana silaha za nyuklia yanaruhusiwa kuhalalisha silaha zao kwa nadharia ya "kuzuia," ambako kuna maana ya kuzuia vita kati ya nchi zenye nyuklia. Lakini ni nadharia ambayo imeshindwa, kwasababu, kama ambavyo tunaona sasa, kama baadhi ya mataifa yanahisi yana haki ya kuwa na nyuklia, mataifa mengine yanadai haki hiyo. Ni mchezo wa kila taifa kuwa na silaha hizo za maangamizi zaidi duniani.

Kinachotakiwa ni kwa mataifa yote kuzingatia sheria moja, ambayo ni kwamba silaha zote za maangamizi – hasa nyuklia, ambazo zinatisha kuliko zote – lazima zikomeshwe.

IPS: Jumuiya za kidini na kiroho zinaweza kufanya nini kufikia changamoto ya kukomesha silaha hizi za maandamizi?

SW: Tunaliona suala la silaha za nyuklia kama moja ya masuala makubwa ya kimaadili katika nyakati zetu. Ni suala ambalo dini za dunia zitahitaji haswa kulishughulikia kwasababu silaha za nyuklia ni silaha za maangamizi zaidi na zinazotisha kupita kiasi kuwahi kutengenezwa.

Hivyo tunaona watu ambao wanapenda na kuwa na nia kuhusu masuala ya kimaadili, kuwa na wajibu wa kutoa wito wa kukomeshwa kwa silaha za nyuklia.

IPS: Kama daktari unayefanya kazi, ni hamasa gani umeipata kulichukulia suala la kuachana na silaha za nyuklia kwa dhamira kama hiyo, na ni kitu gani kimechochea ari yako ya kuhakikisha dunia inakomesha nyuklia?

SW: Silaha za nyuklia zinaangamiza mno. Zinafanya jambo tunalolifanya kama madaktari la kuokoa maisha ya mtu mmoja kwa wakati kuonekana la mzaha. Silaha hizi zinatishia maelfu ya maisha ya watu mara moja na hata vizazi vijavyo.

(END/2010)

 

Search