Kutoka Ajenda Rahisi ya Vita Hadi Mipango ya Amani

AddThis

Nuclear Abolition News | IPS
Mutsuko Murakami


TOKYO (IPS) - Mutsuko Murakami anamhoji IKURO ANZAI, mkurugenzi wa heshima wa Makumbusho ya Kyoto kwa Ajili ya Amani Duniani.

Kati ya wastani wa makumbusho ya amani 170 ambayo yanapatikana duniani kote, theluthi yanapatikana nchini Japan.

Makumbusho ya Kyoto kwa Ajili ya Amani Duniani katika Chuo Kikuu cha Ritsumeikan, mjini Kyoto, yanavuta hisia za historia ya uvamizi wa nchi hiyo ikiwa ni pamoja na uzoefu wake wa wakati wa vita.

Anayeonekana kuwa nguvu kubwa nyuma ya Makumbusho ya Kyoto ni Dk Ikuro Anzai, ambaye pia ni mkurugenzi wake. Akiwa ni mhitimu wa udaktari, alikuwa mwalimu katika shule ya udaktari kabla ya kukaribishwa kufundisha masuala ya kimataifa katika Ritsumeikan mwaka l986.

Dk Anzai tangu wakati huo amepata kutambuliwa na wanazuoni maarufu katika mafunzo ya amani na anatumika kama mkurugenzi wa heshima wa Taasisi ya Nanjing ya Utafiti wa Amani Kimataifa katika Chuo Kikuu cha Nanjing, China.

Mwaka 2008, Makumbusho hayo yalifanya Mkutano wa Kimataifa wa 6 kuhusu Makumbusho kwa Ajili ya Amani, ambao ulivuta zaidi ya washiriki 5,000 kutoka zaidi ya nchi 50. INMP inapanga kuwa na mkutano mwingine wa kimataifa mwaka 2010 huko Barcelona, ambao utafuatiwa na mwingine miaka miwili ijayo mjini The Hague.

Katika mahojiano na IPS, Profesa Anzai anajadili umuhimu wa makumbusho kwa ajili ya amani katika harakati za kutafuta amani duniani ikiwa ni pamoja na matarajio na changamoto zilizopo.

Q: Ni kwa nini Japan ina makumbusho mengi kwa ajili ya amani?

A: Kutokana na nchi yetu kujiingiza zaidi katika vita, iliacha makovu mengi, bila hata kutaja mambo ya kukumbuka kuweza kuoneshwa. Kabla ya vita na kwasehemu kutokana na watu wa (Japan) kuwa na uzoefu wa majanga ya mashambulizi ya nyuklia [akiwa na maana mabomu ya atomiki ya Hiroshima na Nagasaki], watu walijenga hamasa kubwa ya amani mioyoni mwao.

Mwaka 1978 Wajapan walikusanya saini milioni 30 kwa ajili ya Mkutano wa Kwanza wa Upokonyaji Silaha wa Baraza Kuu la Umoja Mataifa. Wamekuwa nguvu kuu wakitaka serikali za wilaya na miji kutokuruhusu nyuklia au kujenga makumbusho ya amani katika miji yao mikubwa kwa midogo. Hakika, mashirika ya kiraia nchini Japan yameonyesha uwezo wao wa kujenga amani.

Q: Unasema makumbusho ya amani yanaweza kufanya kazi kubwa zaidi ya kuweka kumbukumbu na kuonyesha ukweli wa kihistoria kuhusu vita na madhara yake na mateso kwa mwanadamu. Ni jukumu gani linatekelezwa na makumbusho ya amani katika jambo hili?

A: Kukuza "amani" na kuchangia kwa ufanisi zaidi katika kujenga amani duniani, makumbusho yanaweza kuandaa midahalo, kuonesha filamu, jitihada za utafiti, matembezi, mikutano ya amani na maonesho ya utalii, miongoni mwa mambo mengine. Tunaweza kujenga mtandao wa makumbusho hayo na kusaidiana kwa ajili ya lengo la pamoja pia.

Q: Ni sababu gani nyingine zilihamasisha makumbusho katika mwelekeo huu mpya?

A: Tumeona kukua kwa dhana ya amani tangu Dk. Johan Galtung – mwanazuoni wa Norway na mwanzilishi wa mafunzo ya amani – alipofasili miaka ya l970. Amani siyo tu kukosekana kwa vita, anasema, lakini pia kila aina ya unyanyasaji, kunyimwa haki za binadamu, matumizi ya mazingira au kukiukwa kwa tamaduni. Tumehamisha msisitizo wetu katika makumbusho yetu kutoka ajenda rahisi ya kupinga vita na kuingia katika mafunzo mapana ya amani. Baadhi ya makumbusho ya amani pia yamerekebisha fasili hii mpya ya amani.

Q: Ni mambo gani yamefikiwa katika Mkutano wa Kimataifa wa Makumbusho kwa Ajili ya Amani wa Mwaka 2008? Hatua inayofuata ni ipi? A: Kwa kuongeza katika mafanikio ya mkutano wenyewe, ilipelekea sisi kujenga mfumo wa chombo chake cha maandalizi, INMP. Tumeifanya kuwa taasisi ya kisheria, imeunda katiba yake, imeteua viongozi wake, imejenga mfumo wake wa wanachama na kuanzisha ofisi ya kiutawala mjini The Hague. Profesa Peter van den Dungen wa mafunzo ya Amani katika Chuo Kikuu cha Bradford (nchini Uingereza) anakaimu nafasi ya mratibu wake mkuu. Mchakato huu wa kiutaasisishaji unatupatia mwanzo imara wa kuendelelea zaidi katika siku zijazo. Kupitia INMP, tunaweza kuimarisha umoja wetu, kupanua mafunzo yetu ya amani kwa kushirikiana (na taasisi zinazofanana na hizo) na kusaidia makumbusho mapya kuanzishwa. (END/2010)

 

Search